Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 14, 2015

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars Sylvester Marsh amefariki dunia



Sylvester Marsh, enzi za uhai wake akiteta jambo na kocha aliyewahi kuinoa Taifa Stars, Kim Poulsen
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa  Taifa Stars Sylvester Marsh amefariki dunia jana alfajiri katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kocha huyo aliyefanya kazi na makocha mbalimbali wa kigeni alifariki dunia wakati akihudhuria kliniki ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua wa saratani ya koo.


Familia ya Marsh ilisema hali ya kocha huyo ilibadilika ghafla siku tatu zilizopita kabla ya mauti hayajamkuta.

Itakumbukwa kwamba Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jamal Malinzi alipoingia madarakani alibadilisha uongozi ikiwemo kuondoa benchi la ufundi.

Marsh ndiye kocha wa kwanza kuipandisha Azam FC ligi kuu Tanzania Bara mwaka 2007, pia amewahi kuzipandisha ligi kuu Toto Africans (1998), Geita Gold Mines na Kagera Sugar.

Enzi za uchezaji wake dimbani alikuwa nafasi ya mlinzi wa kati, akizitumikia Coop United, JKT, Mzizima, RTC Kagera, Polisi Mara, Tusker FC (Kenya) na Iganga Town Council (Uganda)

Alizaliwa mwaka 1957, hadi mauti yanamkuta alikuwa na kituo cha michezo Marsh Athletes Centre jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment