Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo akiaga mwili wa
marehemu Marsh.
Vijana walio katika Kituo cha soka cha Marsh Academy kilichokuwa
kikiongozwa na marehemu wakishusha jeneza la mwalimu wao kwenye Uwanja wa Shule
ya Msingi Milongo tayari kwa kuaga.
Mke wa marehemu (wa pili kushoto) akilia kwa simanzi. Wa
kwanza kushoto ni binti wa marehemu aitwaye Anna Marsh na kijana wake Wyne
Marsh (wa tatu kushoto).
Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo viongozi wa serikali
wakishiriki kumuaga marehemu Marsh.
Mmoja wa wadhamini wa kituo cha marehemu kutoka nchini
Ujerumani akitoa salamu za rambirambi.
Nahodha wa timu ya vijana ya U-16 katika kituo cha marehemu
akisoma historia ya Academy yao.
...Nahodha huyo akikakabidhi historia hiyo kwa Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Kocha Marsh alifariki dunia Jumamosi iliyopita katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akitokea Mwanza baada ya
hali yake kuwa mbaya.
Mamia ya watu wakiwemo viongozi wa kiserikali, wadau wa
soka, wanasoka na mashabiki wamehudhuria mazishi hayo yaliyoanzia katika Uwanja
wa Shule ya Msingi Milongo ambapo marehemu Marsh na vijana wake walikuwa
wakifanyia mazoezi.
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu lilianza asubuhi katika
uwanja huo baada ya mwili kuwasili kutoka katika Hospitali ya Seketule
ulipokuwa umehifadhiwa.
Vijana waliokuwa wakifundishwa na Marsh katika Kituo cha
soka cha Marsh Academy ndiyo waliopewa jukumu la kubeba jeneza la mwalimu wao.
Wanasoka wa zamani akiwemo Edibily Jonas Lunyamila na Fumo
Felician ambao waliwahi kucheza soka na marehemu kabla ya kuwa kocha walimwaga
machozi wakati wa zoezi la kumuaga mwenzao.
Wasanii wakiwemo Steve Nyerere na H-Baba nao wameungana na
waombolezaji kumuaga mwalimu Marsh.
Sylvestre Marsh aliyezaliwa miaka 55 iliyopita, licha ya
kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars tangu enzi za Marcio Maximo hadi Kim
Poulsen, pia aliwahi kuwa kocha wa timu kadhaa zikiwemo Azam FC na Kagera
Sugar.
(PICHA ZOTE NA JOHNSON JAMES / GPL, MWANZA)
No comments:
Post a Comment