Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 19, 2015

TAARIFA YA KANUSHO TOKA KWA NAPE NAUYE KUHUSU KUZICHAPA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA



 TAARIFA KWA UMMA
Naomba nitumie nafasi hii kukanusha uongo ulioenezwa na wahuni kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Nangole walichapana makonde leo. Uongo huo umeandikwa leo Machi 17, 2015 saa 16:34 PM na kusambazwa kwa mara ya kwanza kupitia IP.21.372.11.7 katika tower namba 4.
Suala hilo ni uongo wa dhahili wenye malengo mahsusi ya kuwachonganisha viongozi hao wawili 
 
ambao kwa pamoja wanaendelea kufanya kazi nzuri ya kuijenga CCM mkoani Arusha kupitia ziara ya Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
Mambo yakudhihirisha kuwa huo ni uongo ni kwamba leo wakati uongo huo unaandikwa huku ukionesha kuwa vurugu na ugomvi huo umetokea katika Hotel ya Naura Spring jijini Arusha, Viongozi wote hao wawili hawajafika kabisa katika jiji hilo.
Kwani kwa wiki nzima wamekuwa katika wilaya za pembezoni za mkoa wa Arusha yaani Monduli, Ngorongoro, Karatu na leo Longido ambapo mpaka muda huu wanaendelea na mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Leo viongozi wote watalala hapa Longido mjini na wala sio Arusha mjini kama uongo huo unavyosema.
Naomba watanzania puuzieni uongo huo ambao hauna mbele wala nyuma.
Viongozi wote wawili yaani Ndugu Nape na Ndugu Onesmo wameonesha ushirikiano mkubwa saana katika ziara ya katibu mkuu wa CCM inayoendelea mkoani Arusha na wala hawajapishana kwa maneno na hata kunyosheana kidole.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Umma
CCM Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment