Kuna taarifa imesambaa sana mitandao ya kijamii hasa Facebook, Twitter na Instagram na pia watu wengine wamekuwa wakitumiana picha ya mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba aka Vengu Whatsapp kuandika "RIP Vengu". Msanii huyu wa kundi la Orijino Komedi ni muda mrefu hatujamuona akiigiza pamoja na kundi lake kutokana na kuumwa.
Kwa taarifa tulizozipata kupitia uongozi wa kundi hilo baada ya kuwasiliana na Seki pamoja na Joti ni kwamba wamekanusha na kusema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa za msanii huyo kufariki.
No comments:
Post a Comment