Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali kwenye red carpet wakati wa sherehe ya siku ya wanawake duniani iliyowakutanisha wanawake kutoka kila kona ya visiwani Zanzibar ambayo iliandaliwa na Kikundi cha Wanawake cha Zanzibalicious na kufanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hoteli ya Bwawani. |
Mbunifu wa mavazi kutoka bara Mama wa mitindo Asia Idarous (kushoto) akipozi na mbunifu wa mavazi kutoka visiwani Zanzibar Matilda Ishungisa wa Malty design.
Makamu mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious, Zaning'ha Otembo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Wanawake wa Zanzibalicious Bi. Evelyne Wilson.
Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe Thuwaiba Kisasi.
Wanaume nao hawakubaki nyuma kutoa sapoti kwa wanawake.
Mama wa mitindo Asia Idarous aking'ara kwenye red carpet.
Kutoka kushoto ni Make up artist Sada, Mama wa mitindo Asia Idarous na MC wa sherehe ya siku ya wanawake duniani visiwani Zanzibar, Mishi Bomba ambaye pia ni mtangazaji wa Magic FM.
Mke wa Naibu Waziri wa Afya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Zakhia Kombo (kulia) akiwa na Mama wa mitindo Asia Idarous. Kwa picha zaidi bofya link hii
No comments:
Post a Comment