Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 30, 2015

BAADA YA KUUWAWA RAIA NANE NCHINI INDONESIA MATAIFA MBALIMBALI YAONYESHA HASIRA

Watuhumiwa nane waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya wameuawa jana Jumanne usiku kwa kupigwa risasi. Raia saba wa kigeni ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Austalia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Gabon ni miongoni mwa waliouawa kwa kupigwa risasi katika jela ya Kisiwa cha Nusakambangan.
Raia mmoja kutoka Ufilipino, Mary Jane Fiesta Veloso ambaye ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu ya kifo amenusurika na adhabu hiyo katika dakika za mwisho.
Kama walivyotangaza, viongozi wa Indonesia wametekeleza adhabu hiyo ya kifo usiku wa manane jana Jumanne. Waliopigwa risasi ni raia wawili wa Australia ambao walikuwa viongozi wa Kundi la Bali Nine, Andrew Chan na Myuran Sukumaran, Zainal Abidin raia wa Indonesia, Rodrigo Gularte wa Brazil, Sylvester Obiekwe Nwolise, Raheem Agbaje Salami na Okwudili Oyatanze wote raia wa Nigeria pamoja na Mghana Martin Anderson.
Pamoja na mashinikizo mbalimbali za kimataifa na maombi kutoka kwa ndugu na jamaa za watu hao waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa ajili ya msamaha, Jakarta ilibakia na msimamo wake mpaka mwisho.

 
 Rais Joko Widodo, ambaye aliingia madarakani katika majira ya joto kufuatia sehemu ya kampeni yake ya kupambana na madawa ya kulevya, ambapo alisema kutowasamehe watu watakaojihusisha na madawa hayo ya kulevya. Utekelezaji wa adhabu kwa watu hao waliohukumiwa ulikuwa unatarajiwa.
 Katika dakika za mwisho, mmoja kati ya watu hao waliohukumiwa kifo, mwanamke ambaye ni raia wa Ufilipino amenusurika kuuawa, jambo ambalo limewashangaza wengi.
 Rais Joko Widodo ameahirisha utekelezaji wa adhabu ya kifo kwa raia huyo wa Ufilipino baada ya kujisalimisha na kudai kuwa alikuwa akijihusisha na biashara ya binadamu.
 Lakini uamuzi huo wa kuahirisha utekelezaji wa adhabu hiyo ni wa muda mfupi kwa raia huyo wa Ufilipino pamoja na Serge Atlaoui, raia wa Ufaransa, ambaye aliondolewa katika dakika za mwisho kwenye orodha ya watu ambao walikuwa wanatarajiwa kuuawa.
 Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbot amelaani mauaji hayo na kuyaita muaji ya kinyama na amemtaka balozi wake kuondoka nchini Indonesia baada ya raia wake wawili kuuwawa baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kusafirisha dawa za kulevya.
Brazil pia imelaani hatua ya kuuawa kwa raia wake mmoja, huku Mataifa ya Magharibi pamoja na Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yamekuwa yakitoa wito kwa Indonesia kutotekeleza hatua hiyo bila mafanikio. Indonesia imetetea uamuzi wake na kusema inapambana na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini humo.

No comments:

Post a Comment