Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 30, 2015

PICHA - MWANAMKE ADAIWA KUBAKWA NA WANAUME ZAIDI SABA SHINYANGA, AZIMIA, ALILEWA POMBE ZA KIENYEJI!!


Mwanamke akiwa hajitambui ndani ya gari la polisi baada ya kudaiwa kubakwa na wanaume zaidi ya saba( tumeficha sura kwa sababu ya maadili)-picha zote na Veronica Natalis
Chumba kinachodaiwa kutumika kufanya unyama huo
Nyumba ya mama Seni
Wananchi wakiwa eneo la tukio

 
Baadhi ya watu waliokamatwa na polisi wakipandishwa kwenye gari la polisi
Mama Seni akipandishwa garini - Picha zote na Veronica Natalis
Kuna stori zingine ukizisikia unaweza kufikiri ni utani ama ndoto!!
 Hii  ya leo imetokea mkoani Shinyanga,ambapo Mwanamke mmoja ambaye anasadikiwa kuwa mkazi wa mtaa wa Matanda katika manispaa ya Shinyanga amefanyiwa vitendo vinavyoelezwa kuwa ni ubakaji na wanaume saba tofauti hali iliyosababisha kupoteza fahamu.


Tukio hilo limetokea leo katika mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga katika nyumba ya mama aliyefahamika kwa jina la mama Seni ambaye anajihusisha na biashara ya kuuza pombe za kienyeji. 

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanamke huyo ni miongoni mwa wateja wa pombe za kienyeji waliofika kwa mama Seni na baada ya kulewa alianza kuvutwa na wanaume ambao pia ni wateja waliokuwa wamelewa.


 Wamesema kutokana na hali hiyo ilimlazimu mwenye nyumba ambaye ndiye muuzaji wa pombe za kienyeji kumuingiza mwanamke huyo chumbani pamoja na wanaume waliokuwa wanamvuta ambao ni zaidi ya 7 .

"Huku kwenye pombe hakuna adabu kabisa,unaambiwa miongoni mwa waliombaka wamo vijana wenye nguvu ,watanashati zaidi ya saba,basi wakamfanyia ukatili ,tunaomba jeshi la polisi litende haki,waliotenda ukatili wapo na wanajulikana kabisa,tunataka wachukuliwa hatua za kisheria",mashuhuda waliongeza.

Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli Roja Mshana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ametowa wito wa wananchi hasa wanawake kujiepusha na unywaji wa pombe wa kupindukia ili kuzuia vitendo vya ukatili kwa wanawake vinavyoendelea kutokea.

Mwandishi wa habari hizi amefika eneo la tukio na  kushuhudia gari la polisi likiwachukua wanaume watatu wateja wa pombe za kienyeji, muuzaji wa pombe hizo aliyehafamika kwa jina la mama Seni  pamoja na mwanamke aliyefanyiwa vitendo hivyo ambaye inasadikiwa kuwa alikuwa amepoteza fahamu.

No comments:

Post a Comment