Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 23, 2015

PAMBANO LA MAYWEATHER NA PACQUIAO , PROMOTA ASEMA MKATABA HAUJASAINIWA

Bob Arum amesema Mkataba wa pambano hilo haujsainiwa bado
PROMOTA wa Manny Pacquiao, Bob Arum amesema kwamba Mkataba wa pambano lake na Floyd Mayweather mjini Las Vegas haujasainiwa ikiwa zimebaki siku kabla ya kukutana ulingoni.
Huku wawili hao wakikamilisha maandalizi yao kwa ajili ya pambano lao la MGM Grand Mei 2, Promota wa Top Rank, Arum ameiambia ESPN kwamba Mkataba bado haujakamilishwa.
Tiketi za pambano hilo pia bado hazijaanza kuuzwa na Arum amesema kwamba, nakala ya Mkataba aliyopelekewa Aprili 15 haikuwa ile ambayo walikubaliana na Mayweather Promotions na MGM wakati wa kusaini makubaliano ya vipengele vya Mkataba miezi michache iliyopita.
"Tulikubaliana kwamba wote tutakuwa watia saini katika Mkataba wa mwisho na wametutumia nakala ambayo haitujumuishi sisi,"amesema Arum.
Kutokuwa watia saini, itamaanisha kwamba Top Rank haitakuwa na maamuzi kwenye mambo kadhaa kama video na muziki wakati wa pambano.
"Hawataki sisi tuwe na kauli yoyote,"amesema Arum. "Hivyo hata wakija na Mkataba baina ya Mayweather na MGM kabla au baada ya makubaliano yetu, kuna mapungufu, ambayo ni kinyume na makubaliano,".
Mtendaji Mkuu wa Mayweather Promotions, Leonard Ellerbe amesema Arum 'hayuko tayari kuwa na makubaliano'

 
Lakini Leonard Ellerbe, Mtendaji Mkuu wa Mayweather Promotions, amepingana na Arum, akisema; "Ukweli wa mambo ni kwamba, Bob hayuko tayari kuwa na makubaliano yaliyosainiwa miezi kadhaa iliyopita, ambayo hayampi fursa ya kuwa na mamlaka,".
Amesema Arum anawasiliana na wanasheria wake kujaribu kubadili vipengele vya Mkataba, tofauti na makubalino ya awali.
22 Apr 2015 

No comments:

Post a Comment