Kamanda wa Polisi wa wilaya ya kipolisi Gongo la Mboto
jijini Dar es Salaam, JCN Simba, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya
afya na sayansi shirikishi ya chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala (KIU),
kampasi ya Dar es Salaam, huko Gongo la Mboto nje kidoho ya jiji Jana Jumanne
Aprili 15, 2015.
Wanafunzi wote kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa tano
wanaochukua shahada, stashahada na vyeti, kwenye taaluma za madawa, pahamasi,
na maabara, wamegoma jana, wakipinga chuo hicho kuendesha kozi hizo bila ya
kuwa na cheti kutoka baraza la wafamasia la wizara ya afya na ustawi wa jamii,
kama sheria inavyotaka.
Ingawa chuo hicho kimesajiliwa na tume ya vyuo vikuu (TCU),
lakini sheria inataka chuo hicho kipate cheti cha kutambuliwa kozi inazotoa
hususan katika masuala ya tiba kutoka kwenye baraza hilo.
Akizungumzia mgomo huo, Mkurugenzi wa mawasiliano wa chuo
hicho, Uki Keneth, alikiri shule hiyo kutokuwa na cheti hicho, lakini akaelezea
juhudi za chuo toka mwaka 2012za kuhakikisha cheti hicho kinapatikana,
zinafanikiwa.
Hata hivyo alisema, chuo kina barua ya kuruhusiwa kuendesha
kozi hizo kutoka baraza ingawa kisheria barua hiyo haina uzito wowote wa
wanafunzi wanaohitimu masomo ya sayansi ya afya chuoni hapo kitambuliwa katika
soko la ajira.
Chanzo: KhalfanSaid Blog
No comments:
Post a Comment