Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 2, 2015

SHAMBULIO LA KIGAIDI LAUA 6 NA KUJERUHI 30 KENYA

WATU wawili wamepoteza maisha huku takribani 30 wakijeruhiwa baada ya watu wapatao watano wanaodaiwa kufunika nyuso zao kushambulia Chuo Kikuu cha Garrissa kilichopo Kaskazini mashariki mwa Kenya.


Baadhi ya wanafunzi waliokuwa chuoni hapo.

Shambulio hilo linadaiwa kufanyika mapema leo wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa katika sala yao ya alfajiri.


Watu walioshuhudia tukio hilo wameeleza kuwa kuna majeruhi wengi ndani ya chuo hicho.

Wapiganaji hao wanadaiwa kuwa ndani ya chuo hicho mpaka sasa wakiwa wamewateka nyara watu kadhaa huku Jeshi la Kenya na maofisa wa polisi wakiwa tayari katika eneo la tukio kukabiliana na watu hao.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kutekeleza shambulio hilo japo Kundi la Wapiganaji wa Somalia, Al Shabaab likihusishwa kufanya shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment