Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, April 6, 2015

Soma Hii::Huenda na wewe hukutarajia hii ingetokea kwa mtu aliyekamatwa kituo cha Polisi






Labda isingekushtua kusikia tukio la mtuhumiwa kuuawa baada ya kukamatwa na watu wenye hasira, lakini hii ya mtuhumiwa kukutwa amefariki akiwa mikononi mwa Polisi iko tofauti kidogo.

Mara nyingi tunaona watuhumiwa wakikamatwa, baada ya kufikishwa kituo cha Polisi wanasachiwa na kuacha kila kitu kwenye meza ya Askari ili kama ana kitu kibaya asijidhuru akiwa amefungiwa jela, uliwahi kudhani kwamba kuna mtuhumiwa atakuja kujiua 


kwa nguo zake alizoingia amezivaa?

Imetokea Masvingo Central Police, kituo cha Polisi kilichopo Zimbabwe ambapo mtuhumiwa mmoja amejinyonga akiwa ndani ya jela ya kituo hicho cha Polisi kwa kutumia T-shirt aliyokuwa amevaa, mtuhumiwa huyo alikuwa amekamatwa kwa makosa ya kumbaka mtoto wa kaka yake, kumpa ujauzito na kumuambukiza HIV.

Jamaa huyo Nevison Tapesana alikutwa akiwa amejinyonga siku moja tu baada ya kufikishwa na kuhojiwa kuhusu mashtaka hayo kwenye Kituo hicho.

Police walishtuka kumkuta asubuhi akiwa ananing’inia dirishani huku akiwa amejinyonga kwa T-shirt ambayo aliingia nayo akiwa ameivaa.

Tapesana anahisiwa pia kuhusika na tukio la kubakwa na kuuawa mwalimu mmoja wa Chuo, hiyo ilitokea kama mwezi mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment