Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 3, 2015

SUMATRA Wanataka Mabasi ya Dar - Mwanza Yatumie Spidi 80 tu


Siku moja baada ya Wakala wa Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kutangaza kupungua kwa mwendo kasi wa mabasi yaendayo mikoani hadi kufikia spidi 80, wasafiri jijini Mwanza wamekumbana na adha kubwa ya kukosa usafiri baada ya mabasi kutoka Dar es Salaam kushindwa kufika kwa wakati mjini hapa. 
 
Katika stendi kuu ya mabasi eneo la Nyegezi jijini hapa, wasafiri hao walisema kauli hiyo ya serikali itawaumiza, hivyo wameiomba kuwasaidia kwa kuisihi iruhusu safari kwa mwendokasi wa kawaida, vinginevyo wao ndiyo wanaopata maumivu.
 
Walisema walikata tiketi mapema lakini wameshindwa kusafiri kutokana na msongamano mkubwa wa watu na hata wakipanda, magari hayo hayaondoki.
 
Mmoja wa mawakala wa mabasi ya kampuni moja, alisema hatuwezi kuendelea kuharibu magari yao kisa spidi 80, hivyo ni bora wakaegesha magari yao kusubiri ya serikali yatakayokuwa na spidi 80 ili yafanye kazi hiyo.
 
Madereva wa magari hayo, ambao walikataa kuondoka stendi licha ya abiria kupanda, walisema ni vigumu kwa mabasi hayo yenye spidi 180, kusafiri kwa mwendo unaotakiwa na SUMATRA kwani kwa kufanya hivyo magari hayo yataharibika mapema.
 
“Serikali ni wavivu wa kukagua magari mabovu ambayo kwa asilimia kubwa ndiyo yanayosababisha ajali na pia kwenye haya magari, baadhi ya madereva hawajakidhi viwango, wao wanatakiwa kuwakagua hawa ili wabaki wenye vigezo, kusema magari yaende kwa spidi 80 ni kujisumbua kwani hakuna mmiliki atakayekubali,” walisema baadhi yao.

Mpaka mwandishi wa habari hizi anatoka kwenye stendi hiyo majira ya saa 5 asubuhi hakuna basi hata moja lililokuwa limewasili kutoka jijini Dar.

No comments:

Post a Comment