Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, April 21, 2015

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA MABIBO WAMLILIA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akikagua Mazingira ya Soko la ndizi la Lililopo Mabibo akiwa ameambatana na Viongozi wa wafanyabiashara wa soko hilo  alipofika kusikiliza kilio chao.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ametembelea Soko hilo mara baada ya viongozi wa soko hilo kufikisha kilio chao cha muda mrefu  kwake na Ndipo alipoamua kufika mara moja kuwasikiliza.Wafanyabiashara hao kilio chao kikubwa kwa Mkuu wa wilaya hawajui hatma ya biashara yao Sokoni hapo kwa kuwa  eneo wanalofanyia biashara sio rasmi kwajili ya soko  ni Mali ya Kiwanda cha Urafiki.Wafanyabiashara hao wakimweleza zaidi Mkuu wa wilaya wamesema Kutokana na kutokutambulika kwa eneo hilo kama eneo la soko kunawanyima fursa mbalimbali ikiwemo Mikopo kwa kuwa eneo hilo halitambuliki.Wafanyabiashara ambao wapo takribani 10000 hao wakieleza zaidi walisema wako hapo kwa muda mrefu lakini hawajui hatma ya maisha yao.Pia Miundombinu ya Soko haifai kabisa hali inayosababishwa kutokutambulika kama sehemu ya soko.
 Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipatiwa Maelezo zaidi kuhusu eneo la Soko hilo kutoka kwa Mwenyekiti wa Soko Hilo Ndugu Idd Pazi kwa niaba ya Wafanyabiahara wa Soko Hilo.

 
 Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Ndizi lililopo Mabibo .Aidaha Mkuu wa Wialya wakati akijibu amewaambia amepokea kwa mikono Miwili Kilio chao Atalifanyaia kazi kwa haraka kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za Maamuzi na Mapema atawajibu.Mkuu wa Wilaya akieleza zaidi amesema Ngumu sana kwake  kutoa ahadi ambayo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa Eneo hilo ni Mali ya Kiwanda cha urafiki na kiwanda kimebinafsishwa ni ngumu kuaahi kama watalipata eneo hilo kwajili ya Soko Bila kujua Mipango ya Kiwanda kuhusu eneo hilo. 
 Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda alitumia Mkutano huo na Wafanyabiashara kuwaeleza Mipango na Mikakati yake iliyokwisha kuanza na ambayo ataianzaisha hivi karibuni kwajili ya Kutatua kero zinazowakabili wakazi wa wilaya ya Kinondoni.Akieleza Zaidi Mh Makonda amesema kwenye ofisi yake kila siku ya Jumanne ni  siku ya Kumwona Mkuu wa Wilaya kwahiyo ametoaa rai wa wakazi wote wa kinondoni wenye matatizo Mbalimbali Kufika ofisini kwake kila Jumanne Kumwona.Pia kwa wale wakazi wa Kinondoni wenye migogoro ya Ardhi Kufika ofisini kwake kila siku ya Ijumaa yuo kwajili ya kutatua kero za wanakinondoni
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko hilo wakimsikiliza kwa makini 
 Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Wakati ikajibu baadhi ya Kero za wafanyabiashara hao.
 Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Baadhi ya Zawadi alizopewa na wafanyabiashara wa Soko la Ndizi la Mabibo.

No comments:

Post a Comment