Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa), Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora
katika Bara la Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa
na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam .
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora katika Bara
la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji mengine
mbalimbali.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Jumuiya
ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United Cities and Local Government of Africa-
UCLGA) na kupewa jina la Rais wa Angola 'President Jose Eduardo Dos Santos-
Africa Mayors Award' ni za mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.






No comments:
Post a Comment