Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwepo kwa mtu mmoja
mwanaume aliyetambulika kwa jina la EXAVERY S/O MICHAEL, Miaka 19, Mkazi
wa Kingugi Mbagala, aliefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akiwa
katika harakati za kuvuka mto Kizinga, na kufikia idadi ya Watu 13 waliopoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari ya mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
Tukio hili lilitokea tarehe 13/05/2015
majira ya saa nane kamili mchana huko maeneo bonde la Mto Kizinga Kata ya
Kiburugwa Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam. Maiti yake iliopolewa na
wasamaria wema na imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi na
utambuzi.
Nawashukuru wananchi kwa namna wanavyojitolea na kushiriki kushughulikia
maafa yanayoendelea kutokea ikiwa ni matokeo ya mafuriko yaliyosababisha na
mvua zinazonyesha mfululizo katika jiji la Dar es Salaam.
Nawaomba wakazi wa maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam waendelee kuchukua
tahadhali kwa kuwa madhara zaidi yanaweza kutokea kutokana na kwamba mvua
bado zinaendelea kunyesha. Aidha, waendelee kutoa taarifa pindi wanapoona hali
yoyote isiyo ya kawaida ili hatua za haraka ziweke kuchukuliwa.
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
S. H. KOVA
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment