SERIKALI imesema itaanza kutekeleza ahadi yake ya kutoa elimu ya sekondari bure katika mwaka wa fedha 2015/16.
Taarifa
hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi,
Celina Kombani wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lushoto,
Henri Shekifu (CCM).
Katika
swali lake, Shekifu alitaka kujua kama tangazo hilo la Serikali la
kutoa elimu ya sekondari bure ni la kweli na utekelezaji wake utaanza
lini.
Kombani alisema tangazo hilo ni la kweli na utekelezaji wake utaanza katika mwaka wa fedha 2015/16.
Awali
akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kibaha Mjini, Francis Koka (CCM),
Kombani alisema uanzishwaji wa Mfuko wa Elimu ni wa kisheria ambao
unawataka wadau mbalimbali ndani ya wilaya kuchangia mfuko na fedha
zinazokusanywa zinatumika kuboresha elimu kulingana na vipaumbele vya
halmashauri husika.
“Sambamba
na uanzishwaji wa Mfuko wa Elimu, uboreshaji wa mfuko huo unafanyika
kwa kutumia asilimia tatu ya mapato ya ndani ya halmashauri .
“Kupitia
mifuko hii, imeanzishwa Mamlaka ya Elimu nchini ambako mwanachama
huchangia Sh 500,000 kwa mwaka na kuweza kuomba fedha za kuboresha elimu
katika maeneo ambayo wanayapa kipaumbele,” alisema.
Aliupongeza
Mji wa Kibaha ambao tayari una mfuko wa elimu ambao umewezesha
kupatikana kwa madawati 500 na ujenzi wa maabara katika shule za
sekondari za Miembasa na Mwambisi.
Katika
swali lake, Koka alitaka kujua mpango wa Serikali wa kuboresha Mifuko
wa Elimu iliyoanzishwa katika halmashauri kwa lengo la kuboresha elimu.
No comments:
Post a Comment