Mshambuliaji
kutoka Argentina anayechezea Manchester City Sergio Aguero amesema ametulia
City licha ya Real Madrid kuonesha dalili za kumtaka. Aguero, 27, anataka
kuchukua Klabu Bingwa Ulaya na City (Daily Mirror) Paris St-Germain watapambana
na Manchester City katika kumwania kiungo wa Juventus Paul Pogba, 22. PSG wapo
tayari kutoa pauni milioni 70 wanazotaka Juve (Daily Star), winga wa Manchester
United Nani, 28, aliyecheza kwa mkopo Sporting Lisbon msimu uliopita, atahamia
Fenerbahce ya Uturuki kwa uhamisho wa pauni milioni 6 na mkataba wa miaka minne
(Sun), Petr Cech, 33, amefikia makubaliano ya kujiunga na Arsenal kutoka
Chelsea baada ya kuhakikishiwa kuwa atakuwa kipa namba moja (Daily Mirror),
kuwasili kwa Cech kutasababisha David Ospina, 26, kuhamia Fenerbahce kwa pauni
milioni 4 (Times), Crystal Palace wameambiwa lazima walipe kiasi kisichopungua
pauni milioni 15 kumsajili Loic Remy, 28, kutoka Chelsea (Daily Telegraph),
mshambuliaji wa Chelsea Patrick Bamford, 21, aliyecheza kwa mkopo Middlesbrough
msimu uliopita, ataanza mazoezi na Chelsea baada ya kukataa kuhamia Newcastle
United (Times), Tottenham wanafikiria kumchukua kipa wa Genoa, Mattia Perin, 22
(Sun), Southampton
hawatomuuza Nathaniel Clyne, 24, kwenda Liverpool chini ya
pauni milioni 15. Tayari wamekataa dau la pauni milioni 10 (Daily Telegraph),
beki wa Liverpool Martin Skirtel, 30, amekubali mkataba wa miaka mitatu na
kumaliza wasiwasi wa kuondoka katika klabu hiyo (Times), Liverpool
wamekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Charlton, Joe Gomez, 18 ambaye
anatafanya vipimo vya afya siku ya Ijumaa (Daily Mail), Chelsea wanamtaka
kiungo wa Zenith St Petersburg, Axel Witsel, 26, kuziba nafasi ya John Obi
Mikel, 28, ambaye anakaribia kuondoka Stamford Bridge
(Daily Express), meneja
wa Inter Milan, Roberto Mancini anamtaka beki wa kulia wa Chelsea Filipe Luis,
na Chelsea wamesema wapo tayari kusikia dau lao (Gazzetta dello Sport),
Arsenal, Liverpool na Southampton wanatajwa kumwania Sven Bender wa Borussia
Dortmund (Bild), Inter Milan imetoa euro milioni 18 kumtaka Gannielli Imbula,
ingawa Marseille wanataka euro milioni 20 (RMC), Liverpool wamewaambia
Manchester City kuwa hawatoweza kumpata Raheem Sterling kwa pauni milioni 40
msimu huu (Daily Mirror). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema-
Cheers!
No comments:
Post a Comment