
KIUNGO wa Barcelona, Xavi Harnandez ametambulishwa rasmi na kablu yake mpya Qatar, Al Sadd kwa mkataba wa miaka miwili.
Raia huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 35 amesema anajua kuna wakongwe wengi wamepita katika klabu hiyo, kwahiyo ataendelea kujifunza kuhusu mpira pamoja na tamaduni za hapo , huku lengo kubwa likiwa ni kuendeleza ubingwa.
Xavi ameondoka Barcelona akiwa ameishindia timu yake vikombe 25 katika miaka 17 aliyoichezea klabu hiyo ya Hispania.
No comments:
Post a Comment