Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 6, 2015

Wabunge 35 wa UKAWA Wafukuzwa Bungeni


Wabunge  35 wa kambi ya upinzani bungeni juzi walitolewa nje ya ukumbi wa bunge na spika wa bunge  Anne Makinda na kupewa adhabu ya  kutokuhudhuria vikao vitano kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge .
 
Mara baada ya kikao cha bunge kuanza spika wa bunge alinza kwa kuwakumbusha wabunge namna ya kufuata kanuni hasa pale wanapotaka kuondoa muswada wowote.
 
Hali ilibadilika ghafla Bungeni baada ya Mbunge Ezekiel Wenje kuomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?
Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… ndipo spika aliamua  kuwatoa nje.
 
Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni  ya sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania iliwasilishwa Bungeni.
 
Majina ya Wabunge waliotimuliwa  ni,
  1. Ezekiel Wenje
  2. Mussa Kombo
  3. Masoud Abdallah Salim
  4. Rebecca Ngodo
  5. Sabrina Sungura
  6. Khatib Said Haji
  7. Dr. Anthony Mbassa
  8. Maulidah Anna Valerian Komu
  9. Kulikoyela Kahigi
  10. Cecilia Pareso 
  11. Joyce Mukya
  12. Mariam Msabaha 
  13. Grace Kiwelu
  14. Israel Natse 
  15.  Mustapha Akonaay
  16. Konchesta Rwamlaza
  17. Suleiman Bungura 
  18. Rashid Ali Abdallah 
  19. Ali Hamad
  20. Riziki Juma
  21. Rukia Kassim Ahmed
  22. Azza Hamad
  23. Khatibu Said Haji
  24. Kombo Khamis Kombo
  25. Ali Khamis Seif
  26. Haroub Mohammed Shamisi 
  27. Kuruthum Jumanne
  28. Mchuchuli
  29. Amina Mwidau
  30. Mkiwa Kimwanga
  31. Salum Baruhani 
  32. Marry Stellah Malaki
  33. Rashid Ally Omary
  34. Mwanamrisho Abama
  35. Lucy Owenya

No comments:

Post a Comment