Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, August 18, 2015

KAULI YA MANJI BAADA YA KUKATWA UDIWANI MBAGALA KUU


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye amekatwa kuwania udiwani Mbagala Kuu, amesema alikuwa ni mgonjwa.
Manji ambaye ameshinda kwa kura nyingi katika kura za maoni, lakini akaenguliwa kwa madai hakuwa katika eneo husika, imesababisha kuzua hasira kwa wananchi wa eneo hilo.
Jana wananchi hao walifika katika Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam wakitaka kujua hatma ya Manji.
Wengi walihoji kwamba Manji amekatwa kwa fitna zinazozihusisha Yanga na Simba ambazo ni klabu kongwe za soka nchini.
“Nilikuwa mgonjwa, inajulikana. Hali yangu haikuwa nzuri, hivyo nisingeweza kufika,” Manji amekaririwa na Salehjembe.

 
Hata hivyo Manji alisisitiza, asingependa kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado linasikilizwa ndani ya chama.
“Nafikiri tuache kwanza, subira ni jambo zuri sana,” alisema Manji.

No comments:

Post a Comment