Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, August 18, 2015

LIVERPOOL WAITANDIKA BOURNEMOUTH GOLI 1 BILA






Majogoo wa Jiji Liverpool wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya AFC Bournemouth katika mechi pekee ya ligi kuu ya England iliyomalizika usiku wa jana uwanja wa Anfield.
Bao pekee la kikosi hicho cha Brendan Rodgers limefungwa dakika ya 26' na straika wake mpya, Christian Benteke akimalizia pasi nzuri ya Jordan Henderson
Unaweza kusema Benteke amefungua akaunti ya magoli Liverpool kwani amefumania nyavu katika mchezo wake wa kwanza.
Hata hivyo, Phillipe Coutinho alifunga goli la kuongoza, lakini refa alikataa  kwasababu Mbrazil huyo alikuwa ameotea.

No comments:

Post a Comment