Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 14, 2015

MGEJA,GUNINITA WANGATUKA CCM ,WAJIUNGA CHADEMA

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa (habari  hawapo pichani )juu ya kungatuka katika chama hicho na kujiunga na Chadema  katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Kulia ni John Gudinita.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, John Gudinita akitangaza kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema jana majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. kushoto Sheik Rajab Katimba na kulia ni Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.
Aliyekuwa.Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja akionesha kuwa yeye ni chandema kwa sasa.

 
Wandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja wakati akitangaza kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema jana majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja amengatuka uanachama wa CCM pamoja kujiuzuru nafasi  ya Uenyekiti wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,Mgeja amesema kuwa ametafakari sana na kuona aungane na chama hicho.

Mgeja amesema kuwa anaondoka kwenda kutafuta mabadiliko katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuongeza kuwa wametumikia chama hicho kwa muda mrefu lakini sasa imefika wakati wa kuondoka.

Aidha amesema kuwa CCM ya sasa imekuwa na vitu ambavyo vinafanywa na watu baadaye kuikigharimu chama kutokana na kuacha msingi wa kukubali maoni ya wanachama.

Wakati huo huo katika mkutano huo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,John Guninita naye amengatuka katika chama hicho na  kujiunga ba Chadema kuongeza nguvu Ukawa.

Guniinita amesema kuwa sasa umefika wakati wa kuondoka kutokana na Chama kuacha kusikiliza wanachama wake na badala yake kuendeleza chuki ndani ya Chama.

No comments:

Post a Comment