Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 26, 2015

MKUU WA WILAYA YA MBEYA ATAKA TAIFA LENYE VIONGOZI WALIOBOBEA KWENYE SAYANSI

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyiremba Munasa akizungumza na viongozi na wajumbe wa Tuiko Mkoa wa Mbeya wakati akifungua mkutano ambao unalengo la kufanya uchaguzi kwa kuwapata viongozi wapya wa Tuiko ngazi ya mkoa katika ukumbi wa chuo cha wafanyakazi (OTU)Kabwe jijini Mbeya .(Picha Jamiimojablog)



Katibu wa Tuiko Mkoa wa Mbeya Ndugu Merbota Kapinga akizungumza katika mkutano huo .

Mwenyekiti wa Tuiko Mkoaa wa Mbeya Daudi Mpolya akizungumza na wajumbe wa mkutano huoambao umefanyika katika ukumbi wa chuo cha wafanyakazi Otu jijini Mbeya Agosti 25 mwaka huu.


Wajumbe wa Mkutano huo wakifatilia kwa umakini hotuba za viongozi wao kabla ya kuingia katika uchaguzi wa kuwachagua viongoizi wapya watakao kiongoza chama hicho kwa awamu nyingine.






Picha ya pamoja.




Na Emanuel Madafa,Mbeya 
MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa, amesema umefika wakati  viongozi ambao wamebobea kwenye masomo ya sayansi wakajikita zaidi kwenye tafiti mbalimbali ambazo zitaiwezesha serikali kuleta mapinduzi ya viwanda hususani kwa nchi kama Tanzania.

Amesema Sekta ya viwanda, ndio sekta pekee inayoweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika  Taifa lolote Duniani.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo leo jijini Mbeya, wakati akifungua Mkutano mkuu na uchaguzi ngazi ya Mkoa wa chama cha wafanyakazi wa Viwanda Biashara, Taasisi za fedha na ushauri, TUICO ambao ulihudhuriwa na wajumbe kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya.

Amesema, Taifa lolote duniani linahitaji watafiti wa kisayansi kwenye Kampuni, Taasisi na katika Viwanda kwani ndio nguzo pekee itakayoleta mageuzi ya kiuchumi ikiwa na kupunguza wimbi la umasikini kwa watanzania walio wengi.

Amesema kwa nchi ilipo fikia  inahitaji kuwa na viongozi bora na imara kwani viongozi imara ndio jibu la masuala yote ya maendeleo iwe kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Aidha, Munasa ametaka wajumbe hao, kuchagua viongozi watakao waletea mafanikio makubwa kwa kutumia watu wa kawaida ikiwa na uwezo wa kuamua  masuala muhimu kwa kundi wanaloliongoza.

Hata hivyo, akitoa neno la kushukuru, mjumbe wa mkutano huo, Charles Lindi, alimuomba kiongozi huyo kutenga muda wa kutoa elimu ya uongozi bora kwa watumishi wa umma na sekta binafsi kwani hotuba yake aliyoitoa imeonyesha uwezo mkubwa wa utawala bora ambao mungu amembariki.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Tuiko Mkoa wa Mbeya Ndugu Daudi Mpolya amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na kujituma zaidi ili kutoa chachu kwa waajili wao kutoa motisha.



Mwisho.

No comments:

Post a Comment