Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 21, 2015

MTEULE WA CCM JIMBO LA MBEYA MJINI AKABILIWA NA KESI YA JINA

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Mbeya Sambwee Shitambala


Na Mwandishi wetu,Mbeya

KESI ya  kuingia kwa jinai  inayomkabili mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi Jimbo la Mbeya mjini, Sambwee Shitambala, imeendelea kusikilizwa jana katika  Mahakama ya Wilaya ya Mbeya.



Shitambala ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, anatuhumiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai baada ya kuvamia na kujenga kwenye eneo la mtu kinyume na sheria katika kiwanja kilichopo eneo la Gombe Jijini hapa.



Kosa hilo  ni kinyume cha sheria ya 266(a) sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 .



 Akisomewa shitaka hilo na Mwendesha mashitaka wa serikali, Wakili Baraka Mgaya, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Girbelt Ndeuluo, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Juni, 2012 na February 2013 katika eneo la Gombe lililopo Jijini Mbeya




Alisema, mtuhumiwa aliingia kwenye eneo la ardhi kiwanja namba 27 na 28 kilichopo katika eneo la Block Bb kata ya Itezi Jijini hapa,mali ya Jaswinda Palsin(Singa Singa) ambaye ni raia kutoka bara la Asia na kujenga nyumba yake ya makazi kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumfanyia maudhi raia huyo.



Hakimu Ndeuro, aliihairisha kesi hiyo hadi September 15, mwaka huu, ambapo upande wa mashitaka utakapoleta watuhumiwa wengine  wanne watakaoungana na Shitambala kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingia kwa jinai kwenye eneo la kiwanja cha Singa Singa huyo.



Hata hivyo taarifa za kuaminika zilizoifikia Blog hii zimeeleza kwamba mgombea huyo pia amevuliwa wadhifa wake wa uwakili kutokana na kuendesha shughuli za kiwakali  zaidi ya miaka mitatu bila ya kulipa kodi ya serikali ambayo ni kinyume cha utaratibu na ukiukwaji wa sheria za maadili katika utumishi wa umma.

  

Mwisho.

No comments:

Post a Comment