Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 20, 2015

WAJASIRIAMALI KUONYESHA BIDHAA ZAO JIJINI MWANZA, SEPTEMBA 26, 2015.

Baadhi ya Wajasiriamali wakiwa katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali kwenye kongamano la wajasiriamali lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden mapema mwaka huu. Kongamano la namna hiyo linatarajiwa kufanyika Septemba 26, 2015 jijini Mwanza  Ukumbi wa  Benki Kuu (BoT), Capripoint.


Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI  zaidi ya 250 wanatarajia kuonyesha bidhaa zao mbalimbali katika kongamano la mafunzo ya ujasiriamali litakalofanyika jijini Mwanza.

Akizungumza na Dar es Salaam leo, Mratibu wa kongamano hilo, Getrude Kilyabusebu alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuwajengea uwezo wajasiriamali hao.

"Wajasiriamali hao katika kongamano hilo watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao mbalimbali na pia watapata mafunzo ya jinsi ya kukuza mitaji yao na mbinu zingine za biashara" alisema Kilyabusebu.

Alisema makongamano ya namna hiyo yamekuwa yakiwasaidia wajasiriamali hao kujuana na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na utengeneza wa bidhaa zao zikiwemo mbinu za ufugaji na kilimo.

Alisema mafunzo hayo utolewa na wataalamu waliobobea katika shughuli za ujasiriamali na matunda ya mafunzo ya  makongamano hayo yamewanufaisha wajasiriamali  wengi wajasiriamali.

Kilyabusebu alisema kongamano hilo lililoandaliwa na  Jumuiya ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (Tanzania Business Entrepreneurs Women) lita Septemba 6, 2015 jijini Mwanza  katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) Capripoint.

Mratibu huyo alisema kuwa pamoja na mambo mengine kila mshiriki atalazimika kuchangia gharama kidogo ili kufanikisha kongamano hilo ambapo katika mafunzo na chakula atatakiwa kulipia sh.30,000, meza ya kuuzia bidhaa na kuzitangaza sh. 20,000 na mafunzo na meza sh.50,000.


Kilyabusebu alitumia fursa hiyo kuwaomba wajasiriamali wa kanda ya ziwa kuweza kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni muhimu kujifunza stadi za kazi zao.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo unaweza kupiga simu namba  0754032589 /0756334078/0673032589.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

















No comments:

Post a Comment