Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, September 21, 2015

BAJAJ WALIYOIKODI WANAFUNZI WA SEKONDARY YA LOYOLA JIJINI DAR ES SALAAM YAGONGWA WANUSURIKA KUFA

 Mwanafunzi wa Sekondary ya Loyola akipelekwa kwenye gari kuelekea Hospitali ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, baada ya bajaj yenye namba za usajili MC 402 AWD waliokuwa wameikodi na wenzake Bandarini wakitokea Zanzibar kugongwa na Pickup Double Cabin yenye namba DFPA 826 katika makutano ya barabara ya Sokoine na Azikiwe jirani na Benki ya NBC. Katika ajali hiyo wanafuzi kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali hiyo.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakimfariji mwenzao Martha Silayo (katikati), aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
 Wananchi wakiangalia bajaj  iliyogongwa. Imeelezwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali wa bajaj hiyo ambapo pia dereva wake alijeruhiwa.

 
 Askari wa usalama barabarani na wananchi wakiwa eneo ilipotokea ajali hiyo.
Bajaj iliyogongwa ikiwa eneo ilipopatia ajali 'Kweli BOGOTI imegongwa'

No comments:

Post a Comment