Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 16, 2015

JALI MBAYA YA MAGARI MAWILI KUGONGANA, YAUA WATU HUKO IRINGA, WENGINE WAJERUHIWA





Gari aina ya Toyota Harrier likitolewa eneo la ajali.

Wananchi wakishuhudia gari hilo wakati likiondolewa eneo la ajali.
Wanausalama wakiwa eneo la ajali.
Toyota Harrier likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiyo. (Picha na Mzee wa Matukio Daima)
WATU wawili wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea  alfajiri saa 11: 30 katika eneo Mizani mkoani Iringa kwenye barabara ya Iringa – Mbeya.
Ajali hiyo imelihusisha lori lenye namba za usajili T 463 CRV lenye tela namba 



T 575 CFD lililogongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Harrier yenye namba IT 997 iliyokuwa ikitokea Dar kwenda nchi za jirani.
Akiongea na tovuti hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea ajali hiyo na kueleza kuwa waliofariki dunia katika ajali hiyo ni waliokuwa kwenye Toyota Harrier ambao ni dereva Utilo Mwanasongole (50) mkazi wa Dar es Salaam na Yona Mwakilasa (22) mkazi wa Ilomba.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa, marehemu alikuwa anajaribu kumkwepa mwanakijiji aliyekuwa akiendesha baiskeli ndipo alipogongana uso kwa uso na lori hilo.
Majeruhi katika ajali hiyo ambao walikuwa katika lori wamepelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment