Maskini! Miss Tanzania
namba 2, 2005/06, Natalia Noel ambaye kwa hivi sasa anaishi katika Jimbo
la Minnesota nchini Marekani, yupo taabani baada ya kusumbuliwa kwa
muda mrefu na ugonjwa wa mfumo wa damu (Lupus Nephritis) na kusababisha
figo zake zote kushindwa kufanya kazi pamoja na moyo wake kuwa mkubwa
hivyo kulala kitandani tu, wakati mwingine akisaidiwa na mashine ya
kupumulia.
Akizungumza kwa tabu kwa
njia ya mtandao kwa nia ya kupata mchango wa matibabu kwa ndugu na
marafiki, Natalia alisema alianza kuumwa ugonjwa huo tangu mwaka 2008 na
mara kwa mara alikuwa akionana na madaktari kwa ajili ya matibabu
lakini ikashindikana.
Alisema kadiri siku
zilivyozidi kusonga, ugonjwa huo ulisababisha kuharibu figo zake na moyo
kuwa mkubwa hivyo kumpa tatizo la kupumua lililosababisha awe kwenye
mashine ya kupumulia mara kwa mara.
“Maisha yamebadilika
sana, zamani nilikuwa naweza kujifanyia kila kitu mwenyewe lakini si
sasa, ugonjwa umenibadilisha sana, kwa sasa natakiwa nisafishwe damu
yangu mara tatu kwa wiki (Dialysis) na zote hizo ni gharama kubwa sana
kwangu, kwani tangu nianze kuumwa fedha zote zimeishia kwenye matibabu,”
alisema Natalia kwa huzuni.
Mrembo huyo alikwenda
nchini humo mara tu baada ya kumaliza mashindano hayo ya urembo na huko
alikuwa akisoma na kuendelea na maisha yake.
No comments:
Post a Comment