Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 18, 2015

PICHA:::DIWANI WA KATA YA UBUNGO KUPITIA CHADEMA APANDISHWA KIZIMBANI


Diwani wa kata ya Ubungo anayemaliza muda wake, Boniface Jacob  amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lisso.
Mbele ya hakimu Hellen Liwa, wakili wa serikali Kenneth Setwao alisema Septemba 11, 2015 katika Wilaya ya Kinondoni mtuhumiwa alitenda makosa mawili.
Katika kosa la kwanza Setwao alisema mtuhumiwa alimpiga mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lisso na kumsababishia maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.



Alisema katika shitaka la pili mtuhumiwa anatuhumiwa kuharibu kamera yenye thamani ya Sh8 milioni, mali ya kampuni ya Uhuru Publications Limited.
Mtuhumiwa anayetetewa na wakili wa kujitegemea, John Mallya amekana mashtaka yote mawili na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza matakwa yaliyowekwa ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi yenye thamani ya Sh8 milioni.



No comments:

Post a Comment