Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 1, 2015

WAFAHAMU MASTAA TZ AMBAO NI NI WATAYARISHAJI, NI WAIMBAJI WA MUZIKI!



Mwimbaji na Mtayar-ishaji wa Studio ya Sharobaro, Bob Junior.PAMOJA na kufanya kazi ya kutayarisha ngoma kali za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva lakini hata wao pia wamewahi kusikia na wanasikika kwenye nyimbo zao au walizoshirikishwa. Over the Weekend inakumegea baadhi yao;


Mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, rapa, Mensen Selekta.JERRY BONIFACE ‘MESEN SELEKTA’
Ni mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva, rapa, mjasiriamali, mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Studio ya De Fatality International. Jamaa aliwahi kutamba na anatamba na Ngoma ya Kanyaboya, Mabele na Nimempata alioshirikishwa na Pamela Daffa ‘Pam D’.



Jamaa amewatengenezea ngoma wasanii kama King Dessa Mo, Kala Jeremiah, Stereo, Joh Makini, Nikki wa Pili, Izzo Biznes, Pah One, G-Nako, Nakaaya, R.O.M.A, Country Boy na wengine kibao.
EMMANUEL MKONO ‘NAHREEL’
Ni mtayarishaji, mwimbaji wa muziki, rapa, mjasiriamali na Mkurugenzi Mtendaji wa Nahreel Entertainment, anatamba na nyimbo kama Usinibwage, Chelewa, Moyoni na zinginezo akiwa na Kundi la Navy Kenzo.
Katengeneza nyimbo za wasanii kama Ridhiwani One, Izzo Bizness, Rama D, Joh Makini, Pah One na wengine kibao.

BIZZMAN
Mtayarishaji na Mwimbaji wa In African Band, aliwahi kutamba na Wimbo wa Mabinti wa Kibongo, Ametoroshwa, Nipe Muda na nyinginezo.Bizzman ni mmoja wa watayarishaji wakubwa na wazuri waliowahi kutokea katika anga la muziki wa Kibongo na kufanikiwa kufanya nyimbo za wakali kibao akiwemo Lady Jaydee, Stara Thomas na wengineo. Ingawa kwa sasa hasikiki kwenye gemu la uimbaji na hata utayarishaji.

JOHN SHARIZA ‘MAN WATER’
Mwimbaji na mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka Studio Combinations, amewahi kusikia akiimba kwenye Wimbo wa Nipende Kama Nilivyo akiwa na Mr Blue, Heshima Kazi na Wife Material akiwa na mtayarishaji mwingine anayejulikana kwa jina la Mbatizaji.Jamaa ametengeneza ngoma kibao ikiwemo ya Mwana, Chekecha za Ali Kiba na nyimbo kibao za 20%.

RAHEEM RUMMY NANJI ‘BOB JUNIOR
Mwimbaji na Mtayar-ishaji wa Studio ya Sharobaro, anajulikana kwa nyimbo zake kama Nichum, Kimbiji, Bolingo, Oyoyo na nyinginezo. Amefanya kazi na wasanii wengi akiwemo Diamond na Wimbo wa Kamwambie.

MARCO CHALI
Mmoja wa watayarishaji matata katika anga la muziki wa Bongo Fleva ameshafanya ngoma kibao ikiwemo, Natamani ya Wakali Kwanza.Sauti yake imewahi kusikika kwenye nyimbo kadhaa ikiwemo ya Party Zone akiwa na AY, Nataka ya Godzilla aliyomshirikisha jamaa huyo, Sijalewa ya kwake mwenyewe na nyingine nyingi.

DULLY SYKES
Mwimbaji na mtayarishaji wa muziki kutoka Dhahabu Records, akiwa amefanya nyimbo kibao za kwake na wasanii wengine ukiwemo wimbo wake wa Togola, Bongo Fleva na nyingine kibao. Amefanya kazi kama mtayarishaji na wasanii kama M 2 the P aliyomshirikisha Young Killer na Dully Sykes mwenyewe ngoma inaitwa Run DSM, Queen Doreen, Diamond na Ommy Dimpoz.

MSWAKI
Ni mwimbaji na mtayarishaji wa muziki, anatamba na Wimbo wa Sofia wa Msanii Ben Pol kama mtayarishaji lakini aliwahi kusikika katika Wimbo wa Open Letter akiwa ameimba baada ya Msanii Albert Mangweha ‘Ngwea’ kufariki dunia na yeye kuimba wimbo huo kwa kuigiliza sauti na michano ya marehemu Ngwea.

No comments:

Post a Comment