Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema chama chake kimepata unafuu mkubwa baada ya kuondoka kwa kada wake mkongwe, Kingunge Ngombare Mwiru, ambaye juzi alitangaza kuachana na chama hicho, akitoa sababu kuwa taasisi hiyo aliyoshiriki kuijenga, imekiuka katiba yake.
Akizungumza
mara tu baada ya Kingunge kutangaza azma yake hiyo katika mkutano na
waandishi wa habari juzi uliofanyika nyumbani kwake maeneo ya Victoria,
jijini Dar es Salaam, Nape alisema wanamtakia kila la kheri huko
aendako, kwani uwepo wake ulikuwa ukikigawa chama.
Alisema
akiwa kama mzee wa chama, kitendo chake cha kuegemea kwa mgombea mmoja
wa urais, kiliwagawa wanachama na kauli zake za mara kwa mara kupinga
maamuzi ya chama, yaliwafanya wanachama wake kugawanyika, jambo ambalo
lilimfanya ageuke kuwa mzigo, ambao haukubebeka.
“Mara
zote tulishindwa kujibu kauli za kushangaza za mzee Kingunge kwa
sababu, tuliogopa kujiabisha kama chama, lakini maadam ameondoka, sasa
tutakuwa tayari kumjibu kwa matamshi yoyote atakayotoa dhidi ya chama,
sasa tutakuwa imara zaidi kuliko awali,” alisema Nape.
Katika
mkutano wake na wanahabari, licha ya madai yake ya chama hicho kukiuka
katika yake, lakini pia alisema lipo hitaji kubwa la mabadiliko
linalotakiwa na vijana, hivyo kwa kutambua jambo hilo, ameamua kuwa bega
kwa bega na vijana hao katika kutaka mabadiliko.
No comments:
Post a Comment