Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 15, 2015

LALA SALAMA YA KAMPENI ZA UKAWA SASA KUTUA PWANI NA KUMALIZIA MBEYA

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vine vinavyounda vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimsalimia Bi. Lemmy Mahogija (albino) na Mtoto wake Zawadi Elias, wakati alipowasili kwenye Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Masumbwe, Jimbo la Mbogwe, Mkoani Geita Oktoba 14, 2015. Mheshimiwa Lowassa na timu yake ya kampeni, wameendelea kuimarisha kampeni zao katika kipindi hiki cha lala salama, ambapo tayari amekwisha zunguka karibi mikoa yote nchini, na anatarajiwa sasa kutua mkoani Pwani na kampeni zake zitakamilika mkoani Mbeya, kabla ya upigaji kura ambapo Watanzania wataamua hapo Oktoba 25, 2015 sawa na siku 11 tu zimesalia. (Picha na Othman Michuzi).
Mh. Lowassa akihutubia maelfu ya wananchi kwenye viwanja hivyo
Mh. Edward Lowassa akifurahi na Mtoto Anne Masanja

 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akihutubia mkutano huo wa kampeni

No comments:

Post a Comment