Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, October 19, 2015

MAGUFULI AZIDI KUIVURUGA KANDA YA ZIWA,AFANYA KAMPENI MAJIMBO YA MAGU, SUMVE, KWIMBA NA MISUNGWI

 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kisesa wakati akiwa njiani kuelekea Magu kwenye mkutano wa kampeni.
 Wakazi wa eneo la kisesa wakifuatilia namna Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alivyokuwa akijinadi wakati akielekea Magu kwenye mkutano wa kampeni mapema jioni ya leo.
Wakazi wa mji wa Magu wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CC Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni kwa ajili ya kujinadi na kuomba kura za kutosha ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi Mkuu wa Urais,Ubunge na Madiwani.

 
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa Magu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mjini humo.
Wakazi wa Magu wakifuatilia Mkutano wa kampeni
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia huku akiwa amesimama juu ya gari katika mkutano wa kampeni mjini Ngudu , wilayani Kwimba, jijini Mwanza, ambapo aliwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
 Wananchi wakishangilia kukubali kumpigia kura Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Misungwi leo
Sehemu ya umati wakazi wa Misungwi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wananchi ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,itakapofika Oktoba 25 mwaka huu.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Misungwi wakishangilia walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt Magufuli
 Mfano wa karatasi la kipigia kura la wagombea urais wa Tanzania Dk Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan.
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Misungwi, Mwanza jioni ya leo, ambapo aliwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli
Magufulika staili bado iko kwenye chati .

No comments:

Post a Comment