Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 21, 2015

MAKAMU WA RAIS AIFARIJI FAMILIA YA RUBANI WILLIAM SLAA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha wageni na kumfariji Meya wa Manispa ya Ilala Mhe. Jery Slaa alipofika nyumbani kwao Gongolamboto jijini Dar es salaam  Octoba 20, 2015 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kifo cha Baba yake Marehemu Rubani William Slaa aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya Hekopta.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa pole kwa wafiwa  nyumbani kwa  marehemu Rubani William Slaa aliyefariki Dunia wiki iliyopita kwa ajali ya Helkopta wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Marehemu Slaa Gongolamboto jijini Dar es salaam Octoba 20, 2015. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment