Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 3, 2015

ORODHA MPYA YA VIWANGO VYA SOKA DUNIANI FIFA, TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 136

Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza viwango vya ubora vya mchezo wa soka kwa mwezi Septemba ambapo Argentina wanaendelea kuongoza katika chati hiyo.

Mabingwa wa dunia Ujerumani wanashika nafasi ya pili, huku Ubelgiji wakishika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora.
Algeria ndio taifa la Afrika linaloongoza likiwa nafasi ya 19 huku Ivory Coast wakiwa nafasi ya 21.
Kwa upande wa Afrika mashariki Uganda wako juu wakiwa nafasi ya 75,Rwanda iko katika nafasi ya 93 huku Burundi wakijichimbia katika nafasi ya 113, kenya wao wako nafasi ya 131 na Tanzania ikiwa nafasi ya 136.
Orodha ya kumi bora
1 Argentina
2 Germany
3 Belgium
4 Portugal
5 Colombia
6 Spain
7 Brazil

 
8 Wales
9 Chile
10 England
Source: BBC

No comments:

Post a Comment