Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 8, 2015

RAIS KIKWETE, BILAL, MAALIM SEIF WAMUAGA MTIKILA

 
Picha ya Mch. Mtikila enzi za uhai wake.
Jeneza la mwili wa Mchungaji Mtikila likishushwa viwanja vya Karimjee kwa kuagwa.
Mwili ukiwa katika jeneza tayari kwa kuagwa.
Rai wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisaini kwenye kitabu cha maombolezo.

 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Maalim Seif Hamad Sharif akisaini kitabu cha maombolezo.
Rais Kikwete (katikati) akiwa kwenye msiba huo kabla ya kuuaga mwili wa Mch.Christopher Mtikila sambamba na viongozi wengine.
Dk.Bilal akiwapa pole wafiwa.
Jaji Francis Mutungi akitoa salamu za pole kwa wafiwa.
Dk.Bilal akitoa heshima  zake za mwisho.
Waombolezaji wakipita kwenye jeneza kuaga mwili wa Mch.Mtikila.
Gari lililobeba mwili wa marehemu  Mch.Christopher Mtikila likiwasili viwanja vya Karimjee, Dar.
Geojina Mtikila, mke wa marehemu akisaidiwa mara baada ya kushuka katika gari lililokuwa limebeba jeneza lenye mwili wa mumewe.
Wanandugu wakiwa wameshikilia maua.
Sehemu ya wanandugu walipokuwa wamekaa wakati wa kuuaga mwili wa Mtikila.
Waombolezaji wakihuzunika wakati wa kuuaga mwili.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Hamad wamejitokezakwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kutoa heshima zao mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila.
Marehemu Mtikila alikuwa mwanasiasa mkongwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Oktoba 4 mwaka huu katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze  Mkoa wa Pwani, wakati akirejea Dar es Salaam kutokea Njombe alikokuwa amekwenda kufanya mkutano wa kampeni.
Viongozi wa vyama vya siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yalipata fursa ya kutoa shukurani zao za pekee kuzungumzia historia ya marehemu enzi za uhai wake ambapo kila mmoja alimzungumzia  Mchungaji Mtikila alivyokuwa kiongozi shujaa, mwenye maamuzi na kusimamia kile alichokuwa akikiamini.
Akitoa salamu za rambirambi Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Jaji, Francis Mutungi amesema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa kwa chama cha DP, kwani alikuwa kiongozi aliyekuwa akisimamia haki na kile alichokuwa akiamini na alikuwa hapindishwi na mtu yeyote na alikuwa ni mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu.
Alisema kuwa Mtikila alikuwa mwanaharakati asiyependa maandamano mwenye kuchukua maamuzi ya kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata haki anayoitaka na ndiye alikuiwa mwanzilishi wa kudai mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Mwili wa marehemu umesafilishwa kwenda Ludewa, Njombe ambapo wakazi wa mkoa huo watapata nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuzikwa. Anatarajiwa kuzikwa kesho.

NA DENIS MTIMA/GP

No comments:

Post a Comment