Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 22, 2015

Ukweli kuhusu milipuko iliyokutwa ndani ya gari la Mgombea Ubunge (Chadema)


Mwanzoni mwa wiki hii kuna taarifa zilienea katika mitandao ya kijamii kwamba gari la Mgombea ubunge kupitia Chadema Musoma mjini Vicent Nyerere lilikutwa na milipuko wakati akifanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyabisale Kata ya Bweli Musoma Mjini, leo Kamishina Msaidizi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Philip Alex Kalangi amezungumza na Ripota wa millardayo.com kuhusu ukweli wa taarifa hiyo.
‘Kuna watu wawili ambao wanafahamika kwa majina ya Goodluck Msuya miaka (42) Dereva wa Mgombea Ubunge Musoma Mjini pamoja na Salum Blein ambae pia ni Mlinzi wa Mgombea Vicent Nyerere wamekamatwa wakiwa na milipuko kumi na tano aina ya Explogel 7M V6 Watergel explosive’- RPC Philip Kalangi
‘Milipuko hiyo ilikutwa kwenye gari la Mgombea Ubunge lililokuwa likiendeshwa na dereva wake kabla ya kukamatwa watu hawa, Mgombea Ubunge Ndugu Vicent Nyerere 


 
alikuwa akiendelea na mkutano ndipo mlinzi wake alikwenda jukwaani na kumpa taarifa kwamba ndani ya gari lake kuna milipuko, Mgombea huyo wa ubunge aliwambia wavipeleke vitu hivyo juukwani na Ndugu Nyerere aliwatangazia wananchi kuwa kuna watu wanataka kumuuwa na wamemtegea bomu ndani ya gari lake’ – RPC Kalangi
‘Katika uchunguzi wa awali wataalamu wa uchunguzi wamesema kweli ilikuwa ni milipuko ambayo kwa wakati huo ilikuwa haijafikia wakati ya kuleta madhara na kutokana na maelezo ya wali dereva na mlinzi wa Mbunge huyo yalitia shaka na ndipo ilipelekea kukamatwa kwani muda wote wao ndio walikuwa na gari hilo na hakuna mtu mwingine alilitumia kwa siku hiyo, kwa sababu sio swala la kawaida tukishagungua kuwa ni mifuko na ukaweza kubeba na kuurudisha’-RPC Kalangi
‘Kuhusu kwamba walikuwa wametega bomu la kutaka kuumua Mheshimiwa hilo bado tunalichunguza kutokana na mazingira ya tukio lenyewe lilivyotokea na tayari Mgombea Ubunge ameshahojiwa ametoa maelezo yake bado tunaendelea kuhoji watu wengine’-RPC Kalangi

No comments:

Post a Comment