Siku ya tatu baada ya Rais Dk Magufuli kuingia Ikulu na kuanza kazi
alifanya ziara za kushtukiza katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
ikiwa ni baada ya kumaliza ziara katika Wizara ya Fedha siku moja baada
ya kuapishwa.
Baada ya kutembelea hospitali ya Muhimbili alifanya mabadiliko ikiwa
kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hussein
Kidantu sambamba na kutaka mashine za CT Scan na MRI zifanyiwe ukarabati
baada ya kukaa miezi miwili bila kuhudumia wagonjwa kutokana na ubovu
wake.
Kamati mpya tendaji ya hospitali hiyo ilikutana jana na mara moja
kuitisha wataalam ambao leo walianza kazi ya utengenezaji wa mashine
hizo.
Taarifa mpya kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel
Eligaisha amesema ni kweli mashine za MRI tayari zimeanza kufanya kazi
na mashine za CT Scan bado zipo katika matengenezo na zitaanza kufanya
kazi wakati wowote kuanzia sasa.
Barua ilisomeka hivi…
NHC YAUNGA MKONO MAENDELEO YA UNUNUZI NA UGAVI KUPITIA KONGAMANO LA KITAIFA
-
ARUSHA-Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linashiriki katika Kongamano la 16
la Mwaka la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi jijini Arusha.
Kongamano hilo ambal...
2 hours ago


No comments:
Post a Comment