Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 11, 2015

Haya ndio makundi ya michuano ya Kombe la Challenge 2015 itakayofanyika Ethiopia


Tukiwa bado akili na macho ya watanzania wengi yapo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi, ambapo Taifa Stars itacheza mechi ya kwanza na Algeria November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, shirikisho la soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA) limetangaza Makundi matatu ya timu zitakazocheza michuano ya Challenge inayotarajia kuanza November 21 na kumalizika December 6.
KUNDI A
  1. Ethiopia
  2. Tanzania
  3. Zambia
  4. Somalia
KUNDI B
  1. Burundi
  2. Djibouti
  3. Kenya
  4. Uganda
KUNDI C
  1. Rwanda
  2. Sudan
  3. Sudan Kusini
  4. Zanzibar
Hata hivyo ratiba ya michuano hiyo bado haijatoka zaidi ya CECAFA kutangaza tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo itakayofanyika Ethiopia. Timu ya taifa ya Kenya ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hilo ambalo walitwaa mara ya mwisho mwaka 2013 Nairobi kwa kuifunga Sudan.

No comments:

Post a Comment