Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 30, 2015

HIZI NDIZO TAARIFA SAHIHI KUHUSU MABUNDA YA NOTI KWENYE NDOO ZINAZENDELEA KUZAGAA MITANDAONI

Habari zilizosambaa mitandaoni kuhusiana na mabunda ya noti za dola ya Kimarekani kuwa zimekutwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa wizi bandarini na TRA sio za kweli, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha.
Ukweli ni kwamba mabunda hayo ya noti yalikamatwa huko jijini York, Portland, Marekani Mwezi Septemba mwaka 2010, na sio hapa Dar es salaam, Tanzania kama ambavyo wadau wengi wa mitandao hasa ya Whatsapp na Instagram wanavyovumisha.
Tumelazimika kutoa habari hii ili kuokoa wadau wetu wengi katika vuguvugu hili la uvumi wa mitandaoni ambayo hupelekea kazi kuwa ngumu kwa wengi wetu tunaotafuta na kutoa taarifa za uhakika na ukweli. Maana samaki mmoja akioza wote huonekana wameoza.
Vile vile hii ni kuwafumbua wale wote wanaohusika kusimamia na kutekeleza sheria ya mitandao wawe macho na kuanza kuchukua hatua madhubuti ili 

 
kupunguza kama si kuondoa kabisa tabia hii mbaya ya kusema uwongo kila kukicha.

No comments:

Post a Comment