Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 10, 2015

MAKAMU WA RAIS, MAMA SAMIA AKABIDHIWA OFISI RASMI NA DKT. BILAL, AKARIBISHWA RASMI NA WAFANYAKAZI WA OFISI YAKE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, jana. Picha zote na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  Nov 9, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, ....baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Makamu wa Rais, wakati akiondoka baada ya makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakiwa wamejipanga mstari wakisubiri kumpokea Bosi wao Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwasili  kwa mara ya kwanza baada ya makabidhiano rasmi ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi ya Maua kama ishara ya makaribisho, kutoka kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, wakati alipowasili kwa mara ya kwanza kwenye Ofisi yake na kupokelewa na wafanyakazi wake .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Sazi Salula,wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi, Nov 9,2015. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Eng. Angelina Madete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza  baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati akiwasili.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowasili kwenye Ofisi hiyo  Nov 9, 2015 baada ya makabidhiano. Akizungumza na wafanyakazi hao Mama Samia, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa bidii ili kutimiza Kaulimbiu ya Mhe.Rais ya 'HAPA KAZI TU'.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao leo alipowasili Ofisini kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi rasmi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wanamama wa Ofisi yake baada ya kuzungumza nao alipowasili ofisi kwake kwa mara ya kwanza  Nov 9, 2015 kwa makabidhiano ya Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu.
---
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekabidhiwa rasmi ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilal Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Baada ya makabidhiano hayo Mhe. Samia, alikaribishwa na watumishi wa ofisi yake ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii kulingana na kauli mbiu ya 'Hapa ni Kazi tu'.

"Kila mmoja afanye kazi kwa bidii mahala pake pa kazi. Wale ambao kauli mbiu ya Hapa ni Kazi tu, itawapita wakae pembeni... watatusamehe", alisema Makamu wa Rais

Aidha Mhe. Samia alisisitiza suala la kuendelea kupendana na kushirikiana miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ili kufanikisha azma ya kuleta matarajio ya maendeleo ya Watanzania wanayotaka kuyaona katika uongozi wa awamu ya tano.

Baada ya kutoa nasaha hizo alifanya kikao na Menenjimenti ya ofisi ambapo alitoa uelekeo wa utendaji kazi katika ofisi hiyo hususan kuzingatia kusimamia masuala ya muungano na mazingira ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Aliitaka Menejimenti hiyo kujipanga upya na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa ajili ya kuleta mabadiliko kwa upande wa masuala ya muungano na mazingira.

No comments:

Post a Comment