Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 4, 2015

MHUBIRI MAARUFU WA NIGERIA TB JOSHUA ATUA DAR ES SALAAM KUSHUHUDIA DKT MAGUFULI AKIAPISHWA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam . TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jana jioni .
Picha na Freddy Maro


Rais mteule wa awamu ya tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli alimpokea Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria  TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jana jioni. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwaMhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam jana  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

No comments:

Post a Comment