Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 4, 2015

TAZAMA PICHA:::MAZOEZI YA KUAPISHWA KUWA RAIS DK MAGUFULI YAPAMBA MOTO JIJINI DAR

 Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho  kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Maofisa mbalimbali  wakiwa katika kibanda cha kiapo wakipanga jinsi viongozi watakavyokaa wakati wa sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

 


 Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
 Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
 Mtu aliyeigiza kama  Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
 Viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa Jukwaa Kuu wakati wa maandalizi hayo.
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na Bendi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa maandalizi hayo.
Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment