Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, November 28, 2015

MSIBA WA KAMANDA MAWAZO WA CHADEMA WAISIMAMISHA MWANZA


Baadhi ya Wakazi wa Mwanza wakiingia kwenye uwanja wa Furahisha


MAMIA ya wakazi wa Mwanza na viunga vyake walijitokeza kwa wingi leo kuja kumuaga aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo,Chadema mkoani Geita,Marehemu Alponse Mawazo.
Tukio hilo la kumuaga Mawazo lilifanyika katika Viwanja vya Furahisha mkoani Mwanza na kushidiwa na viongozi mbali mbali wa Chadema akiwemo Aliyekuwa Mgombea wa Urais Kupitia Chadema ambaye aliungwa mkono na Vyama vya UKAWA,Edward Lowassa,Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Freeman Mbowe, Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu,Fredrick Sumaye,

Safari hiyo ya Mwisho ya marehemu Mawazo ilipelekea shughuli za Jiji la Mwanza kusimama kwa mda kupisha tukio hilo,baada takribani barabara za jiji hili zilijaza watu ambao walikuwa wanakwenda kwenye Viwanja vya furahisha

No comments:

Post a Comment