Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 19, 2015

MWIGULU LAMECK NCHEMBA AZUA GUMZO KUBWA WAKATI AKIAPA BUNGENI TAZAMA HAPA

Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi akiapa mbele ya Spika Job Ndugai.
Mwigulu Lameck Nchemba Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi amezua gumzo Bungeni katika kikao cha Bunge la 11 kilichoketi leo asubuhi wakati Spika wa Bunge Bw.Job Ndugai akiwaapisha wabunge wateule kuwa wabunge rasmi.
Katika zoezi hilo la kuapa ambapo wabunge mbalimbali wamelipitia,kila Mbunge anafika mbele ya Spika na kupewa kitabu chenye maelezo ya kuapia ambapo wabunge asilimia kubwa wamekuwa wakisoma ila ilipofika zamu ya 

 
Nchemba imekuwa tofauti ambapo yeye hakukifungua kitabu chenye maelezo ya kuapaia na badala yake kuapa pasipo kusoma kitabuni.
Mara baada ya kumaliza kuapa wabunge walisikika wakimshangilia kwa kumpigia makofi huku baadhi yao wakisema kuwa ‘amekariri’.“Du,amekariri hadi maneno ya kuapia kweli jamaa kiboko” alisikikika akisema mmoja wa wabunge bungeni hapo.
Mara baada ya kuapa Nchemba anakuwa sasa ni mbunge rasmi ambapo anaweza kuanza kutekeleza majukumu kama mbunge halali wa jimbo la Iramba Magharibi.

No comments:

Post a Comment