Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, November 6, 2015

PICHA 5:::Karim Benzema afikishwa mahakamani kisa mkanda wa ngono

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema amezidi kuingia katika headlines baada ya zile stori za kuvuja kwa kanda ya ngono kuendelea kuchukua nafasi, Jumatano ya November 4 Benzema aliripotiwa kukamatwa kwa kosa hilo ila  November 5 alifikishwa mahakamani.
Karim-Benzema-leave-the-court-house-in-Versailles
Staa huyo wa Real Madrid aliyekuwa akihusishwa kuhamia katika klabu ya Arsenal ya Uingereza katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 ameingia katika kashfa hiyo pamoja na rafiki yake wa utotoni ambaye anacheza naye katika timu ya taifa ya Ufaransa Mathieu Valbuena.

 
Karim-Benzema-C-wearing-a-white-hooded-jersey-arrives-at-the-police-station-in-Versailles
Karim Benzema akiwasili kituo cha polisi November 4
Mshambuliaji huyo inatajwa katozwa faini sambamba na kufungiwa kuonana na mchezaji mwenzake wa ufaransa, hata hivyo ripoti ya kichunguzi kutoka Ufaransa zinasema kosa alilolifanya Benzema lingeweza kumfanya afungwe jela miaka mitano ila taarifa kutoka kwa mwanasheria wa staa huyo Sylvain Cormier ameviambia vyombo vya habari kuwa mteja wake hana hatia.
A-picture-taken-on-November-5-2015-shows-a-car-in-a-caravan-of-police-vehicles-allegedly-transporting-Real-Madrids
Benzema akiwasili mahakamanai leo November 5
Benzema aliyekuwa anasumbuliwa na majeruhi na Mathieu Valbuena waliachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa mapema mwezi huu. Benzema kwa sasa anatoka na Analicia Chaves ambaye alikuwa mpenzi wa staa wa soka wa Ubelgiji  Axel Witsel lakini aliwahi kuhusishwa kutoka na msanii wa pop kutoka Marekani Rihanna.
Karim-Benzema-leave-the-court-house-in-Versailles (1)
Mathieu-Valbuena-Karim-Benzema
Mathieu Valbuena na Karim Benzema

No comments:

Post a Comment