Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 5, 2015

SELENA GOMEZ AWA KIVUTIO UTOAJI WA TUZO!


Mwimbaji Selena Gomez.
Los Angeles, Marekani
MWIMBAJI Selena Gomez juzi aliibuka kwenye utoaji wa tuzo za filamu na kuwa kivutio kikubwa kutokana na gauni alilokuwa amevaa.Selena alikuwa kivutio kwenye tuzo hizo zinazojulikana kwa jina la Annual Hollywood Film Awards, ambazo sherehe zake zilifanyika mjini Beverly Hills, jijini Los Angeles.
Mwimbaji huyo ambaye alikabidhi tuzo ya mchekeshaji bora ambayo ilitwaliwa na Amy Schumer, alishangiliwa sana wakati alipokuwa akipanda jukwaani kutokana na kuvaa gauni refu ambalo lilimtoa kisawasawa.Selena ambaye ametoa albamu yake ya pili mwezi uliopita, alikumbatia Amy mara baada ya kumkabidhi tuzo na kusubiri wapiga picha wamalize kazi yao jambo ambalo pia lilishangiliwa sana.Msanii huyo ambaye amezaliwa mjini Texas, pia alikwenda kupiga picha na muigizaji Alicia Vikander.

No comments:

Post a Comment