Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 23, 2015

HII NDIO LIST YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA ALIYOKABIDHIWA RAIS MAGUFULI




Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na mijadala lukuki kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Wapo wanaharakati na wanasiasa kadha wa kadha wamekuwa wakifanya jitihada za kutaka kutaja majina ya walio nyuma ya biashara hii, lakini mwishoni hupatwa na kigugumizi na kuishia hewani.

Marehemu Amina Chifupa (MB), aling'aka bungeni na kutangaza kwamba anayo majina ya wanaojihusisha na biashara hii haramu na atayataja muda wowote, lakini kwa bahati mbaya akatangulia mbele ya haki kabla ya kutimiza azma yake hiyo.

Rais mstaafu wa awamu ya nne ya JMT, Mhe. Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema amepatiwa majina ya watu wazito wanaojihusisha na biashara hiyo, lakini naye mpaka anaondoka madarakani, hakuchukua hatua zozote.

Yupo Blogger Mtanzania aishiye ughaibuni anayeitwa Mange Kimambi, naye amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuhusu vigogo wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya inayoangamiza vijana wengi na kuharibu nguvukazi ya taifa, lakini mpk sasa Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama nchini vinaonekana kusua sua kulivalia njuga suala hili.

Leo, gazeti la Jamhuri limeandika orodha ya majina ya wanaohusishwa na biashara hii ya madawa ya kulevya ambayo yamekabidhiwa kwa waziri wa mambo ya ndani, Mhe. Charles Kitwanga ambaye ameyafikisha kwa Mheshimiwa John Pombe Magufuli (kwa mujibu wa gazeti hilo).

Je, hii inatoa ishara njema ya 'kutumbuliwa jipu' hili la muda mrefu?

No comments:

Post a Comment