Tajiri huyo anayetambulika kwa jina la Nassoro Ahmed bin Slum
anayemiliki kampuni ya Bin-slum Tyres Ltd, amejitokeza na kukiri kumiliki
baadhi ya makontena yaliyokumbwa na kashfa hiyo lakini amekana kosa
lenye sura ya kukwepa kodi akidai kuwa limefanywa na wakala wake.
“Wafanyabiashara hatuna mamlaka ya kulipa kodi moja kwa moja serikalini.
Tunalipa kodi kupitia kwa wakala aliyechaguliwa na serikali. Mimi
nilimlipa kazi wakala wangu ambaye nimekuwa nikifanya naye kazi kwa
miaka 10,” Bin Slum ameliambia gazeti la Raia Mwema.
“Mara kwa mara huwa ananiletea nyaraka za malipo ya kodi lakini kwenye
mzigo huu wa sasa
ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.
ambao kontena zangu zina matatizo ya kodi, alinitangulizia mzigo na mimi nikamdai nyaraka. Yeye aliniambia ananiandalia faili,” alieleza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wote wanaohusika na kashfa hiyo kukamatwa na kuchukuliwa hatua na kodi iliyokwepwa ilipwe.
Tayari watu 12 wanashikiliwa na jeshi la polisi kufuatia sakata hilo.


No comments:
Post a Comment