Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 3, 2015

WAFANYAKAZI 600 WA TANZANITEONE KUACHISHWA KAZI

KAMPUNI ya madini ya Tanzanite One imetoa likizo ya malipo kwa wafanyakazi 635 kwa lengo la kujiweka sawa katika shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo. 

Wafanyakazi hao wamepewa likizo ya malipo kuanzia jana huku mchakato wa kuwaachisha kazi baadhi ya wafanyakazi ukiendelea kwa kuhusisha pande zote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Iringa mjini, Meneja wa Kampuni hiyo, Apolinari Modest alisema kwa sasa uongozi wa kampuni hiyo tayari ulishafuata taratibu zote za kuachisha kazi wafanyakazi.

Modest alisema hakuna mfanyakazi atakayeachishwa bila ya kufuata sheria na taratibu za kazi kwani uongozi umezingatia kila kitu na kuwataka wafanyakazi kuacha kuwa na wasiwasi juu ya hilo.

 
Alisema mchakato wa kupunguza wafanyakazi umetokana na kampuni kushindwa kujiendesha kutokana na kukosekana kwa uzalishaji kwa muda mrefu na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.
Alisema kwa sasa kazi ya kuchambua wafanyakazi wa kuachishwa iko katika vikao mbalimbali kwa kuhusisha uongozi wa Kampuni ya Tanzanite One, viongozi wa vyama vya wafanyakazi tawi la kiwandani hapo na uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Naye Mwanasheria wa Tanzanite One, Kisaka Mnzava alisema kuachishwa kazi kwa wafanyakazi kutafuata sheria zote za kazi na zitasimamiwa na pande zote na hakuna mfanyakazi atayeachishwa bila kufuata sheria za nchini.
Alisema kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi sio mchakato mgeni katika kampuni hiyo kwani ulishafanyika na hakukuwa na malalamiko yoyote. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Tanzanite One, Daniel Hagay alikiri kuwepo kwa mchakato wa kupunguza wafanyakazi, lakini alikuwa na wasiwasi juu ya taratibu kukiukwa, hivyo kuutaka uongozi kukamilisha kwanza taratibu za kuachisha wafanyakazi ili kila mfanyakazi atayeachishwa awe na haki yake ya msingi.
Akithibitisha hilo, Mkurugenzi wa Sky Group, Faisal Shahbhai alisema kupunguzwa kwa wafanyakazi ni kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko uzalishaji hivyo kushindwa kutekeleza baadhi ya ahadi walizoahidi kabla ya kuchukua kitalu hicho C katika mgodi wa Tanzanite Mirerani wilayani Simanjiro, Manyara.


Alisema mchakato mzima wa upunguzaji wa wafanyakazi utafuata taratibu na sheria za kazi ikiwamo kushirikisha pande zote ikiwemo Stamico, mwakilishi wa serikali kama mbia na viongozi wa wafanyakazi.

Alisema Sky Group imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu tangu ichukue kitalu hicho C kilichokuwa kikimilikiwa na Tanzanite One kutokana na kukosa uzalishaji kwa muda mrefu, lakini pia imekuwa na madeni makubwa ya nyuma.

No comments:

Post a Comment